Hawa hapa wakali wa Bongo Fleva waliochaguliwa kushindania tuzo kubwa Afrika za Soundcity MVP 2020
Tuzo za Soundcity MVP zimerudi tena safari hii kufanyika January 11, 2020, live kutoka jiji la Lagos Nigeria, Kabla ya tukio hilo kuchukua nafasi hii hapa orodha ya wasanii kutoka Bongo Fleva wanaowania vipengele mbalimbali kwenye Tuzo
hizo Diamond Platnumz , Ray Vanny ,S2kizzy, Nandy, Harmonize na Marioo
Diamond Platnumz anaongoza akiwa ametajwa kuwania vipengele 6 Ikiwemo Artist Of The Year, Best Male na Best Collaboration kupitia wimbo wake wa ‘Inama’ RayVanny anamfata akiwa ametajwa kuwania vipengele 3 ikiwemo kipengele kikubwa zaidi cha ‘Song of The Year’,
Marioo ametajwa kwenye kipengele cha Best New MVP, S2kizzy anawania kipengele cha ‘Producer of The Year’, Nandy anawania kipengele cha ‘Best Female’ na Harmonize anawania kipengele cha ‘Listeners Choice Award’ Hii ndio orodha kamili ya Nominees.