Sambaza

‘Muziki wa Tanzania umeniletea umaarufu na kujulikana Duniani’ Christian Bella

MSANII Christian Bella, amesema kuwa ameishi kwenye muziki wa Tanzania kwa muda wa miaka 13, ambao umemfanya awe maarufu na kutambulika duniani, licha ya kuwa bado hajapata Uraia wa kuishi moja kwa moja hapa nchini.

Christian Bella amesema hayo mbele ya waandishi wa habari, wakati anatambulisha Audio na Video ya wimbo mpya, alioufanya na Ali Kiba uitwao Chaku.

“Mimi naishi kwa kibali cha Kazi na Makazi tangu zamani wakati naingia hapa, kwahiyo vigezo vya kupata Uraia ninavyo, nina kila sababu ya kuomba kwa kuwa Tanzania imenitambulisha kwenye Dunia, sikuwa na ustaa nchini kwangu lakini hapa nimepata jina na kupata michongo” amesema Christian Bella.

Aidha msanii huyo ameendelea kusema “Watanzania  walinikubali na kunipa nafasi mpaka leo hii nimetimiza ndoto zangu kadhaa ambazo nilikuwa nazo, siwezi kuweka wazi gharama ninazolipia kuishi hapa ila ni pesa nyingi sana na nalipia kila baada ya miaka miwili” ameongeza.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey