Sambaza

Mkazi Wa Songea Asepa Na Milioni 10 Za Nala Shindano La Mama Kasema

SAMWELY Kisinga, mjasiriamali na mkazi wa Songea ameibuka kidedea kwenye Shindano la Mama Kasema lililokuwa chini ya kampuni ya kizawa ya Nala iliyo chini ya Benjamin Fernandes.

Kisinga alishinda Sh milioni 10 baada ya kuwazidi washiriki wenzake 20 alioingia nao kwenye fainali iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa kuwasilisha wazo la biashara linalotatua matatizo ya mazingira kwa kutumia takataka kuzalisha sheet za dari (Ceiling board) na mapambo ya gypsum.

 

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori wakati wa makabidhiano ya zawadi hiyo, Fernandes alisema kuwa anajivunia kuwapa mafunzo Watanzania ambao wamepokea mpango wake kwa ukaribu.

“Sisi vijana tunafanya kazi katika mazingira magumu na licha ya kuwa kampuni yetu ya Nala imepata tuzo nyingi kubwa ila inatambua changamoto za biashara jambo ambalo limetufanya turudishe tunachokipata kwa jamii na Samwely anastahili pongezi kwa kushiriki na kushinda wengine wasikate tamaa,” alisema.

Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo alisema kuwa Nala imefanya jambo kubwa ambalo linapaswa liungwe mkono na Watanzania wote kwa kuwapa mtaji vijana na elimu pia kuhusu uthubutu.

“Vijana wengi kwa sasa wana elimu kubwa ila wanashindwa kuwa na ubunifu na Tanzania kuna matatizo mengi ambayo yakitatuliwa inakuwa fursa ya kuwatoa kimaisha, hivyo ni wakati wa kutumia akili kubuni namna ya kutatua matatizo kama ambavyo Nala imeanza na ni muhimu kumpa sapoti pia rais wetu John Pombe Magufuli,” alisema.

Mshindi Samwely alisema kuwa hakutarajia kushinda awali kutokana na ushindani ulivyokuwa ila kwa kuwa ameshinda basi atatumia kuendeleza kiwanda chake.

“Nimeshinda ninashukuru Mungu, nitatumia fedha zote kuwekeza kwenye masuala ya kiwanda ili kuongeza uzalishaji, baada ya mwaka mmoja nitakuwa mbali, huu ni ushindi wa Songea na Tanzania kiujumla,” alisema.

Lunyamadzo Mlyuka na Joel Thomas

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey