Mwanasheria wa Tekashi 69 aweka wazi tarehe ya kuachiwa huru rapper huyo
Tekashi 69 atakuwa mtaani mwezi Julai mwaka 2020, amethibitisha Mwanasheria wake Lance Lazzaro. Tekashi alihukumiwa miaka miwili Jela Jumatano wiki hii lakini tayari alikuwa ametumikia miezi 13.
–
“Daniel atatumikia miezi 7 na siku 12 kwa sababu muda ambao aliutumikia unahesabiwa.” alisema Lazzaro. Akitoka atakuwa chini ya Uangalizi kwa miaka 5 na atatakiwa kukamilisha masaa 300 ya kufanya kazi za kijamii. Pia atalipa TZS 85,000 za Kitanzania kama faini.
Toa Maoni Yako Hapa