Sambaza

Mbosso kukiwasha Dar Live Christmas hii

MSANII wa muziki wa kizazi kutoka Label ya WCB Wasafi, Mbwana Yusuph Kilungi  maarufu kama Mbosso Khan amefunguka kufanya maajabu ya kiburudani kwa mashabiki wake siku ya Christmas Desemba 25, 2019 katika Uwanja wa Taifa wa Burudani  Dar Live.

Kupitia kipindi cha Bongo255 kinachorushwa na +255 Global Radio Mbosso amefunguka na kusema kuwa, amejipanga vilivyo kuudhihirishia umma kuwa yeye ni msanii bora na hayupo kwenye game kimakosa. 

“Nimejipanga vilivyo kukiwasha pale Dar Live Christmas hii nimejiaandaa vya kutosha, nitakuwa naimba na Live Band lakini pia kwa wakati huohuo nitakuwa nafanya Playback kwahiyo utaona sio kazi ya kitoto wartu waje kwa wingi kuona balaa nitakalo lidondosha pale.” Alisema Mbosso

Aidha msanii huyo alisema katika usiku huo uliopewa jina la “Tamu za Mbosso” hatakuwa peke yake bali ataambatana na wasanii wengine kutoka tasnia ya muziki wa Bongo Fleva kwenda kutoa Burudani katika mitaa ya Mbagala ambapo ndipo mahali alipokulia kisanaa msanii huyo.  

“Nitakuwa na wasanii kama Young Killer, Chid Benz, Zee Cute, Enock Bella na wengine wengi ambao tumjipanga kutoa burudani ya kufa mtu.” Alimalizia Mbosso

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Mbosso akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo.
Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey