Sambaza

Jela sio kikwazo kwa Kodak Black: Atoa Milioni 18 kusaidia familia zenye uhitaji Christmas hii

Kodak Black yupo Jela kwa sasa akitumikia kifungo chake cha miaka 4, lakini hakimzuii kusaidia Jamii na familia zenye uhitaji msimu huu wa Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Mwanasheria wake bwana Bradford Cohen ameiambia tovuti ya TMZ kwamba rapper huyo mpaka sasa ameidhinisha kiasi cha pesa ($8,000) milioni 18 za Kitanzania kwa timu yake kununua midoli, baiskeli na zawadi nyingine kwa ajili ya watoto wa Kituo cha Paradise Day Care kilichopo kitongoji cha Broward mjini Florida. Ambapo imeelezwa zitagawiwa kwa watoto toka kwenye familia 70 tofauti.

Pia mpango wake msimu huu ni kusaidia taasisi za Kidini, mashirika ya watoto na familia zenye uhitaji.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey