Sambaza

Ndege aliyokuwamo Lil Wayne yakutwa na madawa ya kulevya na silaha

LIL WAYNE alikuwa moja ya abiria ambao wamekaguliwa kwenye ndege binafsi mjini Miami Usiku wa kuamkia leo Desemba 24, 2019. Umeripoti mtandao wa TMZ.

Maofisa wa FBI na kitengo cha madawa walipewa taarifa za ndege hiyo kuwa na silaha pamoja na madawa ya kulevya, waliisimamisha kwenye uwanja wa ndege wa Miami-Opa Locka Executive kwa ukaguzi.

Kwa mujibu wa mtandao wa Miami Herald, silaha na madawa yalikutwa kwenye ndege hiyo. Mwanasheria wake, Howard Srebnick amesema mteja wake (Lil Wayne) hakukutwa na chochote na aliondoka eneo hilo salama. Bado haijafahamika pia kama wengine walikamatwa au waliachiwa baada ya upekuzi huo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey