Sambaza

Drake aanika wazi kuizika bifu yake na The Weeknd

Kwenye wimbo wake mpya ‘War’ toka kwenye mixtape ya mshirika wa OVO, Oliver El-Khatib iitwayo El-Kuumba Tape Vol. 1 – Drake ameeleza kila kitu.

“OVO XO link up,” amechana Drizzy akielezea uhusiano wao wa sasa kuwa kitu kimoja. Aliendelea “And the boy that sound like he sang on Thriller / You know that’s been my ni**a / We just had to fix things, family, 6 things, we can’t split up.” alimaliza Drake.

Wawili hao wote toka mjini Toronto Canada wamekuwa kwenye dimbwi la kurushiana maneno kupitia nyimbo zao kwa muda sasa, bifu lililoanza tangu mwaka 2012 baada ya The Weeknd kusaini na Republic Records na sio OVO Sound kama wengi walivyotarajia kutokana na ukaribu wao na #Drake kumtambulisha vizuri kwenye muziki.

Toka kwenye kazi bifu likazidi kupakwa mafuta na visanga vya wanawake, hii ni baada ya Drizzy kudaiwa kutoka na Ex wa #TheWeeknd, Bella Hadid.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey