Sambaza

Jux atamani kupata mtoto wa kike, aweka wazi mipango yake

Mkali wa muziki wa RnB Juma Jux amefunguka kuwa anatamani kupata mtoto wa kike kwa sababu anataka amlee kwenye mazingira ya kujitegema zaidi.

Jux amesema sababu za kutaka mtoto wa kike ni anaamini kwenye kuwekeza kwa mwanamke kwasababu atakuwa na uwezo wa kusaidia watu wengine.

“Nimesema mtoto wangu wa kike wa kwanza, ila anaweza akawa hata wa pili kama nikipata wa kiume wa kwanza ila awe mtoto wa kike, nitamlea katika akili ili aweze kujitegemea zaidi, naamini  kwenye kuwekeza kwa mwanamke ili ajitegemee kwa sababu kuna vitu vingi sana vitakuwa vizuri na ataweza kusaidia watu wengi sana” amesema Juma Jux.

“Mwanamke ambaye anaweza kujitegemea atakuwa vizuri kwenye maisha kuliko anayemtegemea mtu, kwahiyo mimi hicho ndiyo kitu ambacho nakiangaliaga sana, hata kwa mtu ambaye nakuwaga naye kwenye mahusiano namuangaliaga kama ana uwezo wa kujitegemea, na hata kama hawezi nitamtengenezea mazingira aweze kujitegemea bila mimi” ameongeza.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey