Sambaza

Drake Afunguka Ukweli Wote Kuhusu Bifu Yake Na Pusha T & Kanye West

Drake amefanya mahojiano ya kufunga mwaka, amekutana uso kwa uso na mtandao wa RapRadar. Katika mazungumzo yake Drizzy amezungumzia bifu lake na Pusha T na Kanye West, Pia mtoto wake (Adonis Graham)

Akianza na Pusha, Rapper Drake amesema kwanza sio shabiki wa Muziki wake kwa sababu umekaa kama muuza madawa ya kulevya. Kwamba alipokuwa na umri wa miaka 16 alihisi (Pusha T) ni moja ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya.

“When I was whatever, 16, thinking that he was the biggest dope dealer in the world serving bricks to all, every corner of America, yeah sure… I was… a fan obviously more so just a fan of Pharrell and The Neptunes. I always wanted to be signed to Star Trak and stuff like that, that was the wave. Now that I’m grown-up, and I know him and the truth, it’s just not as appealing.” alisema Drake.

Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kupatana na Pusha T, hali ilibadilika na kujibu kuwa hana hamu ya kumaliza chochote na mtu huyo, na hawezi kurudi nyuma. Pia bado anaamini Kanye West alitumika na kuwa nyuma ya bifu hiyo.

“[Kanye West] Hapo ndipo mambo yote yalianzia, nafikiri alimtumia mtu ambaye hanikubali pia licha ya kuwahi kukanusha kwenye mahojiano. Nafahamu, kuna kitu kinamkereketa sana na siwezi kukiweka sawa.” Alisema Drake na kusisitiza licha ya tofauti hizo bado anamkubali Kanye na anaheshima kubwa kwake.

Drake pia amekanusha taarifa za kwamba alichelewesha kulianika jina la mtoto wake wa Kiume kisa dili la Adidas kama ilivyoanikwa na Pusha T kwenye ngoma ya “The Story of Adidon” ameeleza sababu kubwa ya kufanya vile ilikuwa ni kuchelewa kwa vipimo vya DNA! kwamba alikuwa haamini kama mtoto yule ni wake na alikwenda kupima vinasaba kubaini.

“Niwe mkweli kwako, nilifanya vipimo vya DNA kwa mtoto wangu, na baadaye majibu yaliporudi walisema vipimo vimeharibika hivyo hawana uhakika kwa asilimia 100 kama mtoto ni wangu. Hivyo nilikuwa kwenye hali flani ya kusubiri yenye uoga ndani yake na sikutaka kuiambia dunia kuwa nina mtoto kumbe sio.

Drake alimaliza kwa kuthibitisha kuwa hayupo tena YMCMB na sasa yupo chini ya Universal Music kupitia lebo yake ya OVO Sound.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey