Sambaza

Idadi Ya Wanaume Ambao Amber Rose Amewahi Kutoka Nao Kimapenzi Itakuacha Mdomo Wazi

Jina lake halisi ni Amber Levonchuck lakini ni maarufu kwa jina la Amber Rose, ni maarufu katika ulimwengu wa shoobiz kutokana na kazi yake ya mitindo na kuigiza.

Lakini inawezekana wengi hawatambui kama hiyo ni kazi yake kwa kuwa zaidi jina lake lilikuzwa kutokana na matukio yake ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu maarufu wa fani mbalimbali.

Kwa sasa umri wake ni miaka 36, ni mama wa watoto wawili wakiume aliowapata kwa wanaume wawili tofauti. Uhusiano wake wa kimapenzi maarufu ulikuwa ni alipokuwa na Kanye West na baadaye Wiz Khalifa, wote hao wakiwa ni wanamuziki wa Hip Hop.

Miaka miwili iliyopita aliwahi kuulizwa kuhusu idadi ya wanaume ambao amewahi kulala nao yaani kufanya ngono au kuwa nao kwenye uhusiano kabisa, alisema hakumbuki idadi.

Kauli hiyo ilipokelewa tofauti lakini ndiyo uhalisia wa maisha yake, wengi walimponda na kuona anajidhalilisha, hoja yake iliyoibuka nayo ni kusema mbona mwanaume akiwa na wanawake wengi jamii inaona sawa, kwa nini inapokuwa kinyume chake jamii ione siyo sawa.

Mpaka sasa bado ni maarufu lakini taswira yake kwenye jamii siyo nzuri kutokana na matukio yake ya kupenda ngono. Hii hapa ni orodha ya wanaume aliowahi kuwa kwenye uhusiano wa muda mrefu au mfupi, rekodi inaanzia mwaka 2008 ambapo ndipo alipoanza kupata umaarufu.

Kanye West

Huyu ndiye alikuwa staa wa kwanza kwake, alianzisha uhusiano naye mwaka 2008, ikiwa ni baada ya Kanye kumuona Amber katika video ya wimbo wa What Them Girls Like wa Ludacris. Wakaanzisha uhusiano wa siri baadaye Kanye akamuweka hadharani na hapo ndipo umaarufu wake ulipopaa kwa kasi.

Walipendeza kwenye mazuria mekundu mengi kwa kuwa wote ni watu wa mitindo na hawakuficha hisia zao hata mbele za watu. Uhusiano wao ulivunjika na Amber akamtuhusmu Kim Kardashian kuingilia penzi lao.

LeBron James

Nyota huyu wa kikapu katika NBA alikuwa na uhusiano wa muda mfupi na wa siri mwaka 2010.

Reggie Bush

Mchezaji wa zamani wa mchezo wa American football alionja penzi la mrembo huyu mwaka 2010.

Fabolous

Rapa ‘bishoo’ naye alitumia fursa mwaka huohuo kulala na Amber ambaye ni kama alikuwa ameamua ‘kujigawa kirahisi’ baada ya kuachana na Kanye.

Eddie Murphy

Mchekeshaji huyu naye akatumia msongo wa mawazo wa Amber kufaidi penzi alipomkaribisha kwenye mjengo wake wa kifahari mitaa ya Miami.

Darrelle Revis

Mwaka 2010 ulikuwa mgumu na mzuri kwa Amber kwa kuwa pia alilala na nyota huyu wa American football.

Drake

Rapa huyu naye hakulaza damu kama wenzake alijitosa mwaka huohuo.

Amar’e Stoudemire

Mkali wa kikapu katika NBA naye alipewa burudani na Amber Rose mwaka huohuo

Brooklyn Brand

Huyu ni mfanyabiashara ambaye alidumu kwa siku kadhaa tu na Amber mwaka 2010.

Wiz Khalifa

Baada ya kurukaruka sana akakutana na rapa huyu, baada ya mahaba kuwakolea wakafunga ndoa iliyodumu kwa miaka miwili na kufanikiwa kupata mtoto mmoja. Uhusiano wao ulianza mwaka 2010. Walifunga ndoa Julai 8, 2013 wakatengana Septemba 22, 2014 na talaka rasmi ikatolewa Juni 6, 2019.

Angalau huyu alimtuliza kwa muda na akaacha kurukaruka, mtoto wao anaitwa Sebastian Taylor Thomaz.

Rosa Acosta

Hapo katikati akiwa na Wiz pia ilidaiwa kuwa alikuwa akichepuka, iliwahi kuelezwa kuwa alilala na Rosa Acosta ambaye ni mwanamke mwenzake, yaani ‘walisagana.’

Nick Simmons

Huyu ni mwanamuziki na muigizaji, alifaidi tunda mwaka 2014 wakati huo Amber alikuwa hayupo vizuri na Wiz.

French Montana

Staa wa muziki aliruka na bibie mwaka 2014 kwa muda mfupi tu.

Samuel Eto’o

Mshambuliaji wa zamani wa Barcelona na Inter Milan naye aliwahi kufurahia mahaba ya Amber kwa usiku mmoja mwaka 2014, walipokutana kwenye starehe jijini London.

Nick Cannon

Inaonekana mwaka huu wa 2014 ulikuwa wa mvurugano kwa Amber kwa kuwa aliruka hadi na mwanamuziki na mtangazaji huyu.

Quincy

Dansa huyu walifurahia penzi lao mwishoni mwa mwaka 2014.

Chris Brown

Kabla mwaka haujaisha, mwanamuziki huyu naye alifaidi ukaribu wake na Amber.

Orodha ni ndefu lakini wengine maarufu waliotajwa ni hawa hapa:

James Harden

Fani: Kikapu

Mwaka 2015.

Machine Gun Kelly

Fani: Mwanamuziki

Mwaka: 2015

 

Odell Beckham Jr.

Fani: American football

Mwaka: 2017.

 

Eric André

Fani: Muigizaji

Mwaka: 2015.

 

Myles White

Fani: American football

Mwaka: 2016

 

Terrence Ross

Fani: Kikapu

Mwaka: 2016.

 

Joe Budden

Fani: Mwanamuziki

Mwaka: 2016

 

Val Chmerkovskiy

Fani: Dansa

Mwaka: 2017.

 

Offset

Fani: Mwanamuziki

Mwaka: 2017

 

Monté Morris

Fani: Kikapu

Mwaka: 2018

 

21 Savage

Fani: Mwanamuziki

Mwaka: 2018.

Alexander ‘AE’ Edwards

Huyu ndiye baba mtoto wake wa pili na wapo naye hadi sasa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey