‘Siwezi Kubadili Dini Kwasababu Ya Mapenzi’ – Linah
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Linah Ni moja ya wasanii ambao hawawezi kubadili dini kwasababu ya mapenzi. Linah alishawahi kufunguka kuwa pamoja na baba mtoto wake kuwa muislam lakini suala la kubadili dini ili kuivuta ndoa ni swala gumu sana
Linah alisema kuwa “Unajua kiimani hutakiwa kufanya vitu juu juu, hata ukibadilisha dini ni kwa sababu ya Mungu siyo kwa sababu ya mapenzi, kwa hiyo mimi sikutaka kufanya hiyo michezo na ninaamini patalegea popote au tutaoana hivyo hivyo au Mungu mwenyewe atalegeza kwa sababu tunapendana na tayari tuna mtoto”. Pengine Linah aliona mbali kwani mpaka sasa hayupo tena kwenye mahusiano na baba mtoto wake na Linah anatajwa kutoka kimapenzi na Dj wa Harmonize, Dj Seven Worldwide .
Toa Maoni Yako Hapa