Sambaza

Mambo Manne Muhimu Usiyoyafahamu Kumuhusu Nandy

Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’ ni mwanamuziki nyota wa kike anayefanya vizuri sana kwa sasa Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla. Unapotaja jina lake si rahisi kukuta mfuatiliaji mzuri wa sanaa na muziki hajui jina hili.

Leo tunaangazia mambo manne muhimu ya kufahamu kuhusu nyota huyu;


Ni mtu wa kanisani sana
Ukiachana na yeye kujikita zaidi kwenye muziki wa kidunia, historia ya Nandy inaonesha kuwa ni mtu aliyekuzwa katika misingi mikubwa ya imani ya Kikristo. Wazazi wa Nandy ni waumini wakubwa wa dini ya hiyo na mara kadhaa Nandy amewahi kukiri kuwa hata kama anafanya muziki wa kidunia lakini bado anapenda sana kuhudhuria kanisani. Amewahi kunukuliwa akisema kuwa, wakati ukifika ataachana rasmi na muziki wa kidunia na kuingia rasmi kuimba muziki wa injili.

Ana wivu sana
Ikitokea una uhusiano wa kimapenzi na Nandy basi hakikisha unaacha mahusiano mengine yote na kujikita kwake tu. Ni mtu ambaye mara nyingi anapenda kuwa karibu na mpenzi wake. Hata asipokuwa karibu naye, basi atapenda muda mwingine wawe wanawasiliana. Nandy amewahi kunukuliwa katika mahojiano na mtandao wa Millard Ayo akikiri suala hilo hususan wakati akiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Rapa Billnass. Billnas pia amewahi kukiri kuhusu suala hilo. Amewahi kusema kuwa ameshawahi kwenda Afrika Kusini bila kumpa taarifa mpenzi wake kisa ikiwa ni wivu tu!

Hupenda kula
Licha kuwa na mwili mdogo, mwanadada huyo amewahi kunukuliwa akisema yeye na kula ni ‘damdam’. Amewahi kunukuliwa akisema: “Ninakula sana….naweza nikala pleti mbili za wali maini, nkachanganya na mseto halafu nakakaa nusu saa nikala chips na kuku robo.

Mtoto wa baba
Ni mara chache sana kusikia wasanii wanawake kuzungumza kuhusu wazazi wao wa kiume hususan wanaofanya muziki wa kidunia. Mara nyingi husema baba zao huwawekea ngumu wakisikiawanataka kujishughulisha na muziki. Lakini kwa upande wa Nandy yeye na baba yake ni marafiki wakubwa na mara nyingi tu huwa na wanazungumza kuhusu kazi yake ya muziki na mambo mengine.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey