Davido Aporwa Saa Ya Milioni 68 Apagawa Vibaya
Staa wa Muziki wa Afrobeats na mshindi wa Tuzo ya BET Davido aibiwa saa yake yenye thamani ya Dola 30,000 za Marekani (Sawa na TZS Milioni 68) muda mfupi baada ya kufika nchini Ghana.
Kwa mujibu wa mtandao wa GhanaCelebrities saa hiyo iliibiwa baada ya Davido kutoka klabu (Tantra Night Club) iliyopo mitaa ya Osu, Accra, Ghana. Kitendo ambacho kilimfanya msanii huyo kupagawa kutokana na saa yake hiyo ya gharama kubwa kuibiwa kirahisi huku akiwa ameivaa mkononi mwake… .
Katika Video inayoonekana mtandaoni inaonesha jinsi alivyotaka kurudi klabuni kupigana na yeyote aliyeiba saa hiyo ila hakufanikiwa kutokana na kuzuiliwa na watu kwenda kufanya fujo.
Davido alikwenda nchini Ghana kwaajili ya kutumbuiza kwenye tamasha la AfroNation ndipo mkasa huo ukamtokea.
View this post on Instagram