Ex Wa Marehemu Bobbi Kristina Brown, Nick Gordon Akutwa Amefariki Dunia
Nick Gordon amekutwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo akiwa na umri wa miaka 30. Gordon alikuwa mpenzi wa zamani wa mtoto wa Whitney Houston, Bobbi Kristina Brown.
Chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi mpaka sasa japo mtandao wa Time.com umeweka wazi kuwa Gordon amefariki kwa kuzidisha dawa za kulevya na alikimbizwa hospitali mjini Florida siku ya mkesha wa mwaka mpya kufuatia mfululizo wa mashambulio kadhaa ya moyo.
Familia ya Bobbi Kristina Brown alimtuhumu Gordon kuwa mtuhumiwa namba moja wa kifo cha binti yao ambaye alifariki mwaka 2015 kwa matatizo ya dawa za kulevya.
Toa Maoni Yako Hapa