Izzo Bizness Hutumia Masikio Ya Wazazi Wake Kupata Muziki Mzuri
Kawaida ilivyozoeleka, Wasanii wengi huwaweka kando wazazi wao hasa kwenye masuala ya muziki, ila ni tofauti kwa Rapa Izzo Bizness, kwani ameweka wazi kuhusu ushiriki chanya wa wazazi wake kwenye kukuza muziki wake.
Rapa huyo mzaliwa wa Mbeya alisema, kabla ya kuachia wimbo wake wowote, huwa anawatumia wazazi wake wausikilize kwanza na watoe maoni yao,
“Huwa nawashirikisha wazazi wangu kwenye muziki wangu. Kabla sijatoa dude lolote huwa nawatumia wasikilize.” Alisema rapa Izzo Bizness na kuendelea,
–
“Sio kwamba wananichagulia ipi itoke, No, wanachofanya ni kama kuna kitu cha kurekebisha wananiambia, siunajua tena busara zao.”
Toa Maoni Yako Hapa