Sambaza

Drake Afunguka Chanzo Cha Bifu Lake na Chris Brown

Rapa Aubrey Graham maarufu kwa jina la Drake, amefunguka kwa mara ya kwanza chanzo cha mgogoro wake dhidi ya mkali wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown.

Kwenye mahojiano na Podcast ya Rap Radar, Drake, amesema wawili hao waliingia kwenye mgogoro kwa sababu ya Rihanna, lakini anashukuru kila kitu kwa sasa kipo sawa na wamefanikiwa kufanya muziki wa pamoja.

“Chris alikuwa kwenye uhusiano na Rihanna kwa kipindi kirefu hadi wanakuja kuachana mwaka 2009, baada ya kuachana nikawa rafiki wa karibu na Rihanna jambo ambalo halikuwa sawa kwa Chris, lakini hakukuwa na kitu chochote kibaya na ndiyo maana kwa sasa sina tofauti na Chris. “Ukweli ni kwamba wanawake wamekuwa sababu kubwa ya migogoro, nadhani kwa sasa Rihanna atakuwa anaumia akiwa anaona au kusikia kuwa nipo karibu na Chris,” alisema msanii huyo.”

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey