Sambaza

Country Boy – ‘Kuna Wakati Mama Yangu Alinisahau’

Rapa Country Boy amesema moja kati ya changamoto ambazo amezipitia wakati anarekodi album yake ya Yule Boy, ni Mama yake mzazi kusumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili na kupoteza kumbukumbu.

Akiongea na waandishi katika uzinduzi wa Album hiyo, Country Boy amesema Mama yake aliumwa kwa muda wa miezi minne, hali iliyomfanya awe analala masaa matatu kwa muda wa miezi miwili.

Nilikutana nachangamoto kubwa sana wakati narekodi Album yangu mwishoni, Mama yangu alikuwa anaumwa sana karibia miezi minne hivi, alikuwa amepooza akawa anashindwa kutembea, kuongea na kupoteza kumbukumbu hata kuna muda alikuwa hajui mimi ni nani” amesema Country Boy

Aidha Country Boy ameongeza kusema “ilikuwa inanipa wakati mgumu, kuna nyimbo kama 8 zilipotea kwa hiyo ilibidi nianze kurudia, nilikuwa nalala masaa matatu kwa muda wa miezi miwili katika harakati za kurudia nyimbo na kushinda Hospitali

Album yake ya Yule Boy ameizindua rasmi siku ya Januari 3, 2020 jijini Dar es salaam na ina nyimbo 30

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey