Sambaza

Cyril Afunguka Sababu Za Kuachana Na Feza Kessy

Msanii Cyrill Kamikaze, ameeleza sababu iliyomfanya aachane na mrembo Feza Kessy, ikiwa ni pamoja na kutotaka kuweka wazi masuala yake ya mahusiano.

“Kila mtu ana mawazo yake wapo ambao wanaamini nina michepuko, mimi maisha yangu nilichagua kwamba kuna vitu nitaweka wazi na vitu vingine sitaweka wazi vitakuwa private, hasa mambo yangu ya mahusiano, sikutaka hiyo njia labda kwa siku zijazo nitafanya hivyo maana mashabiki wamekuwa wakinilazimisha sana” ameeleza Cyrill Kamikaze.

Aidha Kamikaze ameendelea kusema “Ila mimi nilichagua kila kitu kiwe siri ila sababu hiyo haikuwa ya kuachana wala kuwa wote, kukataa kwangu kuweka vitu wazi kulipelekea kila mtu kuwa na mtazamo wake, hasa issue yangu na Feza Kessy ningependa ibaki siri kama tuna jambo tutamalizana wenyewe, hilo jambo kwa sasa halipo tena, limekatika na haliendelei kabisa” ameongeza.

Pia Cyrill Kamikaze amesema licha ya kuachana kwao sasa hivi wamebaki kuwa marafiki na watu wa karibu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey