Sambaza

Video – Diamond Atoboa Siri Alichomfanyia Rais JPM

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Diamond Platnumz,  ameweka bayana alivyofurahi baada ya kupigiwa simu na Rais  John Magufuli, akiwa katikati ya shoo mkoani Kigoma usiku wa Desemba 31, 2019, alipokuwa akifanya maadhimisho ya miaka yake kumi kwenye muziki.

Mondi ameyasema hayo katika mahojiano yaliyofanyika jana kwenye treni wakati yeye na wanamuziki wenzake waliokuwa Kigoma wakirejea jijini Dar es Salaam ambapo amepongeza rais kwa kazi kubwa anayoifanya ikiwa ni pamoja na kuisapoti tasnia ya muziki nchini. 

“Kabla hatujafika Kigoma, Mheshimiwa Rais aliagiza watu kuja kutusapoti zaidi na kutushika mkono pale tunapokwama. Kama haitoshi yeye mwenyewe alikuwa akitazama shoo yetu hiyo live; sikutegemea kabisa.  Lakini tena akaamua kupiga simu on stage na kutupa moyo akiipongeza tasnia ya muziki na kuwatakia Watanzania heri ya mwaka mpya.  Kwa kweli ni rais wa kipekee sana na haijawahi kutokea.

Kwa sasa hapa Dar es Salaam kuna arena mbili zinashughulikiwa, serikali inatengeneza arena hizo. Ni jambo kubwa sana kwetu sisi kama wasanii. Tunamuombea rais ashinde tena kwa kishindo mwaka huu ili atufanyie makubwa zaidi.

DIAMOND Asimulia RAIS ALIVYOMPIGIA – “SIKUAMINI Kabisa, HAIJAWAHI Kutokea, ARENA Zinajengwa”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey