Sambaza

Dudubaya Agoma Kujisalimisha BASATA, Awatolea Povu

BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) limemtaka msanii wa Bongo Fleva, Tumaini Godfrey, maarufu Dudubaya, kufika katika ofisi za baraza hilo Januari 7 (leo), kwa mahojiano zaidi baada ya kusambaa kipande cha video kikimuonyesha akitoa kauli zisizokuwa na maadili.

Hatua hiyo imo katika taarifa kwa umma iliyotolewa na BASATA jana Januari 6, 2020.

Baada ya wito huyo, Dudubaya amejirekodi kipande cha video na kukirusha kwenye mtandao wa Instagram akisema:

“BASATA nimepata wito wenu na siwezi kuja, kwa sababu huwezi kuniita kuja kunionya kwa kurekodi clip za neno kufi… (tusi, kufanya ngono kinyume cha maumbile), hata mama Rwakatale kanisani huwa anasema kabisa kwamba wasagaji, walawiti wafi….(tusi)  hawataiona pepo.

“Hata katika vitabu vitakatifu Mungu hakufumba amesema kabisa kwamba walawiti wasagaji wafi…(tusi) hawataiona pepo, hata kama namfundisha mtoto wangu nitasemaje? Kufi….(tusi) ni vibaya, nimwambie kupigwa fimbo au?

“Lazima tuheshimiane, mkitaka nije lazima mhakikishe kwamba vyombo vya habari ambavyo vina ugomvi na wasanii, muweke suluhisho la amani ili muziki huu uweze kusonga mbele, siji,” amesema Dudubaya.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey