Sambaza

Gigy Money Hana Mchezo na 2020

Mwanadada mwenye mbwembwe nyingi mitandaoni ambaye pia ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amesema mwaka huu amejipanga kuongeza juhudi katika kazi zake za muziki ili kujiongezea kipato hasa baada ya kuona matunda yake kwa mwaka 2019.

Gigy amesema ni dhahiri kazi zake za kimuziki zimemuweka pazuri mpaka kufikia hatua ya kusaini mikataba ya kuwa balozi wa makampuni mbalimbali hapa nchini.

“Yaani kwa staili hii ya madili tu, basi naahidi ni kazi juu ya kazi kwani nimegundua kuwa hakuna kingine kinachoweza kukupa hela zaidi ya kazi nzuri ambazo zinakubalika na watu,” amesema Gigy.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey