Sambaza

‘Sio Lazima Kila Tukisaidia Tutangaze’ Kim Kardashian

Kim Kardashian amekasirishwa na watu ambao wanataka yeye na familia yake waoneshe kwenye mitandao kila misaada wanayotoa kwa Jamii.

Shabiki mmoja aliibuka Twitter na kumbwatukia Kim Kardashian kwamba wameshindwa kusaidia watu waliokumbwa na majanga kadhaa ya moto ambao umekuwa ukizuka kwenye misitu mbali mbali nchini Marekani na maeneo mengine ya dunia.

“Hakuna kitu kinanitia moto kama kuona familia ya Kardashian na Jenner wakiongelea kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na kuteketea kwa misitu na huku wakishindwa hata kuchangia Senti Moja.”

Kim Kardashian hakumlazia damu, alimjibu kwamba; “Hakuna kitu kinanitia moto kama kuona watu wakijidai kujua kila tunachosaidia na kufikiri kwamba ni lazima tuweke wazi kila kitu.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey