AliKiba Afunguka Kuhusu Ishu Ya Mapenzi
Mfalme wa Bongo Fleva Ali Kiba, ametoa dukuduku lake kuhusu suala zima la mapenzi na kusema mapenzi yanaumiza na wala sio kitu cha mchezo.
Ali kiba amezungumzia uzoefu wake kuhusu mapenzi na kusema kuwa aliwahi kuimba wimbo ambao uligusia uhalisia wa mapenzi yake.
“Ni kweli mapenzi yanaumiza na sio kitu cha mchezo mchezo, haina haja ya kusema kwamba umeumizwa kwenye mapenzi halafu unakaza watu watajua tu, mapenzi sijui kwanini yaani na mimi sitaki kujua, ila kiukweli mapenzi kavu sana hayafai,” amesema Ali Kiba.
Ameongeza kuwa, alishawahi kuandika wimbo kuhusu mapenzi na yaliyomkuta, ila hawezi kutaja ni wimbo gani ambao aliutoa kuhusiana na maisha yake ya mapenzi.
Toa Maoni Yako Hapa