H.Baba Atupa Dongo Gizani
Mwanamuziki Hamis Baba ‘H.Baba’ ametupa dongo gizani na ikidaiwa kuwa ni dhidi ya Diamond Platnumz baada ya msanii huyo kuchapisha andiko ambalo limetafsiriwa kama dongo kwa Diamond Platnumz.
Kupia ukurasa wake wa Instagram, H.Baba ambaye alitamba na nyimbo mbalimbali mwanzoni mpaka mwisho mwa miaka ya 2000 ameandika: “Sicheki nawapiga show za bure tena mnaomba mkaimbe bure mwisho wa siku mnaimba remix nyimbo za watu au zako hawazijui eti mnaitangaza Tanzania unaimba wimbo wa Mkongo unasema wa kwako huo ndio wimbo bora wa mwaka huu show yako umearikwa wewe imba nyimbo zako remix za nini?
Hivi karibuni H.Baba amekuwa akiwasakama wasanii na wafuasi wa WCB Wasafi hususan Diamond Platnumz kutokana na ukarabu wake na Harmonize, ambaye kwa sasa hana uhusiano mzuri wa lebo hiyo.
Harmonize amekuzwa na kulelewa ndani ya lebo ya WCB na baadaye kuamua kujiengua na kufanya kazi zake binafsi.