Sambaza

Breaking: Kobe Bryant Afariki Katika Ajali Ya Helikopta – Video

MCHEZAJI maarufu wa mpira wa kikapu kwenye Ligi ya NBA ya Marekani, Kobe Bryant (41),  amefariki katika ajali ya helikopta iliyotokea leo huko mji wa Calabasas, California.   Helikopta hiyo imeanguka baada ya kuwaka moto angani na watu wote watano waliokuwemo wamefariki.

Taarifa zinabainisha binti wa wa #KobeBryant, Gianna Maria Onore ‘Gigi’ (13) ni mmoja kati ya waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Mkuu wa polisi wa Los Angeles (LA) amesema kuwa hakuna yeyote aliyenusurika katika ajali hiyo.

Ripoti za awali zilisema kuwa kulikuwa na watu watano ndani ya ndege.

Bryant, ambaye ni bingwa wa NBA mara tano,  alikuwa anatambuliwa duniani katika historia ya kuwa mmoja wa wachezaji bora wa vikapu.

Ajali ilitokeaje?

Afisa wa polisi, Alex Villanueva, alisema kuwa helikopta inaonyesha kuwa na watu tisa wakati inaanguka, na kuondoa idadi ya watu watano ambao walitajwa hapo awali na maofisa.

Katika taarifa iliyotolewa na mji wa Calabasas zilisema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa.

“Ndege hiyo ilianguka nje kidogo ya mji wa Las Virgenes majira ya asubuhi wa saa za Marekani. Hakuna aliyenusurika, aliongeza.

Gavin Masak, aliyekuwa anaishi karibu na eneo tukio hilo lilipotokea, alikiambia kituo cha CBS News kuwa helikopta hiyo ilianguka.

“Haukuwa kama mlipuko lakini tulisikia kama bomu limelipuka kwa sauti kubwa. Lakini ilisikika kama sauti ya ndege au helikopta, ilisikika sauti kubwa sana, niliingia ndani na kwenda kumtaarifu baba yangu na kumwambia kilichotokea. Hivyo nilivyotoka nikaona moshi mweusi ukitokea mlimani, ulikuwa mweusi au kama kijivum ” alisema.

Shahidi mwingine alisema kuwa alisikia injini ikiwa ina matatizo hata kabla ndege haijafika chini.

Polisi wa LA wameonyesha picha za tukio la ajali hiyo zikionyesha gari la zima moto na moshi ukifuka kutoka milimani.

Presentational white space

Bodi ya taifa ya usafiri imeitambua ndege iliyoanguka kuwa ni Sikorsky S-76B na imesema kuwa itatuma kikosi chake kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

Bryant alikuwa nani?

Bryant alicheza mpira wa kikapu kwa miaka 20 katika viwanja vya Los Angeles Lakers. Aliacha kucheza mpira huo Aprili 2016.

Mafanikio yake ni pamoja na kuwa mchezaji bingwa wa NBA kwa mwaka 2008, mara mbili aliibuka kuwa bora zaidi ya wengine.

Vilevile alikuwa mfungaji bora wa NBA pamoja na bingwa mara mbili wa mashindano ya Olimpiki.

Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.

Bryant alishinda tuzo za Oscar kama mchezaji wa filamu fupi mwaka 2018 filamu hilo ilikuwa ‘Dear Basketball’, filamu ya dakika tano iliyoangazia barua moja ya michezo aliyoandika mwaka 2015.

Aliwahi kupata pointi 81 dhidi ya wachezaji wa Toronto Raptors mwaka 2006, katika historia ya michezo ya NBA.

Bryant na mke wake, Vanessa, walikuwa na watoto wengine wa kike watatu ambao ni Natalia, Bianca na Capri.

Bryant alishutumiwa kwa kesi ya unyanyasaji wa kingono mwaka 2003, na binti mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akifanya kazi katika mgahawa wa Coloradot. Alikanusha madai hayo na kusema kuwa walikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya kukubaliana.

Kesi hiyo ilifutwa baada ya mtu aliyemshtaki kukataa kutoa ushahidi mahakamani.

Ingawa baadaye aliomba radhi kwa kitendo kile na kusema sababu ilikuwa msichana aliyekuwa naye hakuwa na mtazamo sawa na wake wakati walipokuwa kwenye mahusiano yao.

Watu wanasemaje kuhusu kifo cha nyota huyo?

Salamu nyingi za rambirambi zimemiminika katika mitandao ya kijamii kufuatia taarifa ya ajali hiyo.

Shaquille O’Neal, ambaye alicheza na Bryant huko Lakers kati ya mwaka 1996 na 2004, alisema hana neno la kusema kwa sababu ya maumivu ambayo anayo.

“Ninakupenda na utakumbukwa,” aliandika katika mtandao wa Instagram wakiwa katika picha ya pamoja na jezi zao za Lakers.

Deron Williams, aliyekuwa mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki akiwa na Bryant, aliishiwa maneno. alimuelezeaBryant kuwa mchezaji bingwa aliyewahi kucheza naye.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey