Sambaza

Tanasha: Mondi ataniua

MZAZI mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’, Tanasha Donna amefunguka mambo mengi likiwemo jambo kubwa lililosababishwa na mpenzi wake huyo ambalo liliweka rehani uhai wake, IJUMAA WIKIENDA lina habari kamili.

Tanasha amefunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita, alipokuwa akifanya mahojiano maalum na chaneli ya mtandaoni ya nchini Kenya.

ALIANZA NA EP

Mwanamama huyo alianza kwa kuelezea kuhusu uzinduzi wa EP (nyimbo kadhaa) iliyokwenda kwa jina la Donnatela alioufanya hivi karibuni nchini humo. “Naweza kusema ni mafanikio makubwa. Nimefanya jambo kubwa kwa kusaidiwa na timu yangu, lakini pia kupata sapoti kutoka kwa Diamond,” alisema Tanasha.

AZUNGUMZIA MONDI KUTOWEKA

Kwenye eneo hilo la uzinduzi wa EP, Tanasha aliulizwa sababu za mpenzi wake Mondi kutoweka ghafla saa chache kabla ya tukio hilo, ambapo alisema ni jambo la dharura.

“Ni jambo la dharura kwa sababu asingeweza kuja hadi Kenya, akapoteza pesa na muda wake, halafu aondoke bila kuhudhuria, ilikuwa ni dharura na ni jambo la faragha hivyo nisingependa kulizungumzia,” alisema Tanasha.

UVUMI WAIBUKA

Licha ya Tanasha kutofafanua kwa undani kuhusu kile alichokiita ‘faragha’, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kupitia vyanzo vyake mbalimbali nchini Kenya, liliweza kunasa madai kuwa Mondi alitoweka ghafla baada ya kukwaa skendo ya kutaka kumbaka mhudumu wa hoteli ambayo jina lake halikupatikana mara moja.

SIKU YA TUKIO…

Vyanzo hivyo vilidai kuwa, siku ya tukio, Mondi akiwa hotelini akijiandaa na shoo hiyo, mhudumu huyo alikinukisha kwa kupiga kelele kuwa mkali huyo wa Wimbo wa Baba Lao alitaka kumbaka. “Ilikuwa ni vurugu unaambiwa hadi Tanasha akaitwa, sasa ili kuua soo Mondi akaamua kutoweka fasta. Huwezi kuamini mpaka sasa wanamsaka,” mtoa ubuyu mmoja alilieleza IJUMAA WIKIENDA.

TALE ALIELEZA ANACHOKIJUA

Kuhusu madai hayo, meneja wa Mondi, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ alipoulizwa na IJUMAA WIKIENDA, alieleza anachokijua. Alisema habari hizo ni za kizushi ambazo zina lengo la kumchafua msanii wake.

“Hapo hakuna ukweli wowote, hata sisi tumeziona hizo habari kama mnavyoziona ninyi (IJUMAA WIKIENDA), lakini kifupi hakuna kitu kama hicho,” alisema Babu Tale.

TURUDI KWA TANASHA

Kwenye mahojiano hayo, Tanasha alieleza jinsi Diamond alivyotaka kumtoa roho baada ya yeye kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo ambaye alikuwa na umaarufu mkubwa kuliko yeye. “Ilikuwa ni presha sana kwangu, niliingia kwenye uhusiano wakati mwenzangu yeye ni mtu maarufu sana kuliko mimi. Nikakutana na shinikizo kubwa la maneno mazito kutoka kwa mashabiki wake.

“Nilipata depression (msongo wa mawazo) nilikuwa kwenye hali mbaya sana, sikuwa na uzoefu huo, mashabiki walinisema vibaya mno kwa kweli sikuwa sawa, nilijisemea kama hali ikiendelea hivi huyu jamaa (Mondi) ataniua,” alisema Tanasha.

Kwenye kipengele hicho, Tanasha aliongea kwa uchungu na kudhihirisha kwamba ilifika wakati alijutia kuingia kwenye uhusiano na Mondi kwani bila yeye asingeweka rehani roho yake.

AMSHUKURU MUNGU

Tanasha alisema, anamshukuru Mungu kwamba kwa msaada aliopata kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wanaomzunguka, aliweza kuhimili vishindo hivyo hadi kurejea katika hali yake ya kawaida.

AWAPIGIA SALUTI WABONGO KWA UDAKU

Katika hatua nyingine, Tanasha alisema alichojifunza kati ya Tanzania na Kenya, Bongo udaku a.k.a umbea umeshika hatamu kwenye mitandao ya kijamii ambapo kwa kiasi kikubwa unasaidia kumkuza msanii husika. “Udaku wa Tanzania upo ‘next level’ tofauti na Kenya, natamani na Kenya ifikie hatua ile kama wenzetu,” alisema Tanasha.

TUJIKUMBUSHE

Tanasha alikutana na Mondi mwaka juzi mwishoni na kuanzisha safari yao ya mapenzi ambayo hadi sasa, imejibu kwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Naseeb JR. Kwa nyakati tofauti, Mondi alitangaza kuwa tarehe ya kumuoa mrembo huyo kutoka Kenya, lakini hata hivyo, aliahirisha dakika za mwisho.

Tangu Tanasha ajifungue, hajawahi kusema chochote kuhusu ndoa huku vyanzo mbalimbali vikieleza kuwa kuna fukuto la chini kwa chini linalotaka kumpindua mrembo huyo kwenye himaya yake na kurejeshwa ulingoni Hamisa Mobeto, mmoja wa warembo waliowahi kubanjuka naye.

 

STORI: ERICK EVARIST NA GLADNESS MALLYA, DAR

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey