Sambaza

Mobeto “Mniache Sina Mwanaume Kuongea na Esma Isije Kuwa Nongwa

 

MWANAMAMA anayebeba ‘taito’ tatu kwa mpigo ya uigizaji, mwanamuziki na mwanamitindo, Hamisa Mobeto amesema hana mwanaume na haitaji usumbufu.  Akizungumza na Risasi Vibes, Hamisa amesema anashangaa watu wengi wanajadili suala la yeye kurudisha urafiki na Esma ambaye ni dada wa Diamond, ambapo wanadai kuwa amerudiana na baba watoto wake huyo kitu ambacho si cha kweli.

“Hivi watu kumbe wanapenda watu waishi kwenye ugomvi miaka yote kitu ambacho sio sahihi, ningeomba tu wajue mimi sijarudiana na mtu wala sina mpango huo. Kuongea na Esma sio tatizo maana ni shangazi kabisa wa mtoto wangu na kama tofauti zetu, tuliziweka pembeni,” alisema Mobeto.

Esma na Mobeto walikuwa hawana mawasiliano mazuri kwa muda mrefu lakini hivi karibuni, wameonekana wakiwa pamoja wakifurahia maisha, jambo ambalo limezua gumzo mitandaoni

Stori:Imelda Mtema, Risasi

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey