Sambaza

Ray C Amiss Maisha ya Skendo

WAKATI Bongo watu wakimisi picha za utupu za mastaa kutokana na sheria ya makosa ya mtandao kung’ata wengi, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amejilipua huko majuu.  Ray C ambaye ni msanii maarufu anayeishi nchini Uingereza kwa sasa, ametupia hivi karibuni picha tata kwenye ukurasa wa Instagram na kuzua gumzo.

 “Naona umemisi maisha ya skendo, unajitoa fahamu eee,” komenti ya dada mmoja ilisomeka kwenye ukurasa aliotumia staa huyo wa kitambo kuweka picha hiyo ya nusu utupu. Jicho la mwandishi wetu limeiona picha hiyo aliyoiweka mtandaoni akionekana amekaa kitandani huku akiwa amevaa kinguo kilichoacha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi.

Mbali na kinguo kuacha sehemu kubwa wazi, lakini pia kilikuwa na matundumatundu ambapo wengi walipoiona walisema: “Angekuwa Bongo staa huyo angeuona mkono wa serikali.” Aidha, Ray C hakuonekana kujali komenti za waliokosoa picha hiyo, hata mwandishi wetu alipomtafuta kupitia mawasiliano ya meseji ya WhatsApp kujua kilichomchachua hadi kuweka picha hiyo mtandaoni, hakujibu.

Ray C amepita katika maisha ya ustaa kutokana na kazi yake ya sanaa kabla ya kutopea kwenye matumizi ya madawa ya kulevya, kisha kuachana nayo na kutimkia majuu kula bata. Mara kadhaa ameonekana akiwa krozi na mwanaume wa Kizungu ambaye anatajwa kuwa mchumba wake na kwamba ndiye anayempa jeuri ya maisha kwa sasa

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey