Sambaza

Idadi ya vifo kutokana na Corona yapanda, maambukizi yapungua

Idadi ya waliokufa kutokana na virusi hatari vya Corona nchini China imepanda na kufikia watu 1,483 leo lakini idadi ya maambukizi mapya kwenye jimbo lililoathiriwa vibaya la Hubei imepungua.

Tume ya afya ya jimbo la Hubei imeripoti vifo 116 zaidi na visa vipya 4,823 vya maambukizi ya Corona vingi vikijumuisha wagonjwa waliotambuliwa kutokana na dalili pekee.

Hapo jana jimbo la Hubei, ambalo ndiyo kitovu cha mripuko wa virusi hivyo ilirikodi vifo 242 na visa 14,800 vya maambukizi huku idadi jumla ya wale waliogundulika na virusi hivyo nchini China imefikia watu 64,600.

Maafisa wa afya wa jimbo hilo wamesema wameanza kuwatibu wote walioonesha dalili za kupatwa na virusi badala ya kusubiri vipimo vya maabara kuthibitisha kuwa wana ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona unaofahamika kama COVID-19

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey