Rapper A.K.A Kaomba Collabo Kwa Davido
Kama si mfuatiliaji mzuri wa kinachoendelea mitandaoni basi ngoja nikujuze
Tangu litoke tukio la ubaguzi nchini Afrika Kusini la kuwaondoka wageni na kuwapiga kisha kuharibu mali zao wakiwemo Wanigeria na mataifa mengi
Kitendo hizo kiliwakwaza na kuwaumiza baadhi ya nchini kwa unyama unaofanyika Afrika Kusini
Sasa Nigeria ilikuwa ni moja ya nchi ambayo raia wake walipigwa na kuharibiwa mali zao
Kitendo hicho kilionekana kuwaumiza Wanigeria
Miongoni mwa wasanii waliokuwa wameguswa na tukio hilo ni Davido na Burna BOY ambapo wawili hao walionekana kumrushia maneno mazito Rapper AKA huku wakimuahidi kumfanyia kitu mbaya yaani kumpiga
Burna BOY alionekana kukerwa zaidi na kuahidi kutokwenda tena nchini humo baada ya raia wa Nigeria kufanyiwa ubaguzi
Sasa leo habari nyingine imeibuka ni baada ya AKA kumuomba Davido wafanye wimbo wa pamoja
AKA ameweka wazi matamani ya collabo na Davido kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo aliandika ujumbe unaoashiria anahitaji verse za Davido ili kukamilika kwa wimbo huo
Sasa Wanigeria hawajamuacha hivi hivi AKA wamemvaa kwenye akaunti yake ya twitter na kumpa onyo kali kisha kuikataa collabo hiyo
Huenda Wanigeria bado wana maumivu ya ndugu zao waliotendwa kwenye tukio la ubaguzi ama Xenophobia lililowahi kutokea siku zilizopita huko Afrika Kusini
NA Davido bado yuko Afrika Kusini ambapo wiki iliyopita alikabidhiwa cheti na kampuni ya Sony Music Africa kumtambua mchango wa muziki wake.