Sambaza

Corona Yasogeza Mbele Michuano Ya COPA AMERICA Na EURO

MKUTANO wa kwanza wa kujadili hatima ya michuano ya EURO uliomlazimu Raisi wa UEFA (Aleksander Caferin) kutumia njia za kielektroniki kufanya mkutano huo, umeazimia kusogeza mbele tarehe za kuanza michuano hiyo hadi June 11 – Julai 11, 2021.

Saa chache baada ya UEFA kutangaza msimamo wao juu ya kuhairisha michuano ya EURO ambayo awali ilitakiwa kuanza Juni 12 na kumalizika Julai 12 2020, Shirikisho la Soka la Amerika ya Kusini (CONMEBOL) nalo limesogeza mbele michuano ya COPA AMERICA hadi mwakani 2021.

Ripoti zinasema kuwa fainali za EUROPA na UEFA nazo zitasogezwa mbele mpaka Juni 24 na 27, mwaka huu.

Hata hivyo mjadala mkubwa umezuka baada ya maamuzi hayo kwani michuano ya EURO ilitarajiwa kuingiza mapato mengi yanayokadiriwa kuwa ni Zaidi ya dola za Marekani bilioni 2.5 na huku UEFA wakiwa tayari wamepokea takribani dola milioni 300 za manunuzi ya tiketi ya fainali hizo.

#Tusanue, je unaunga mkono maamuzi ya UEFA?

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey