Sambaza

Nicki Minaj Atajwa Kuwa Rapper wa Kike Tajiri Zaidi Duniani

IKIWA dunia ipo kwenye maadhimisho ya mwezi wa wanawake duniani, huenda tabasamu la Nicki Minaj likarejea tena  baada ya kutajwa kwenye akaunti rasmi ya Young Money kuwa ndiye rapper wa kike mwenye utajiri wa mkubwa Zaidi duniani akiwa na mkwanja zaidi dola za Marekani milioni 100 (sawa na Tsh bilioni 230).

 

Mwanzoni mwa Machi, mwaka huu, mume wa Minaj (Kenneth Petty) alijikuta mikononi mwa polisi kwa tuhuma za makossa ya udhalilishaji wa kingono, lakini baadaye Kenneth aliachiwa huru kwa masharti ikiwemo kuzuiwa kutoka nje ya Kusini mwa California.

 

Hata hivyo Minaj amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa rapa bora Zaidi kuliko rappers wengine wa kike duniani kwa sababu mpaka sasa, anamiliki taji la msanii wa kike namba moja mwenye maingizo mengi zaidi kwenye chati za #billboardhot100.

 

#Tusanue, unadhani ni msanii gani wa kike hapa bongo ndiye rapa bora zaidi?

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey