Sambaza

“Coronavirus” Kuwafikisha Mahakamani Cardi B na Prodyuza Wake

NYIMBO ya Cardi B “Coronavirus” inayofanya vizuri  kwenye mitandao ya kijamii na kumbi mbalimbali za starehe huenda ikampelekea kufungua kesi mahakamani dhidi ya mtayarishaji wa nyimbo hiyo anaetambulika kwa jina la “Imarkkeyz”.

Wiki iliyopita, Cardi B alipata wasiwasi kuhusiana na suala la “coronavirus” hivyo akatumia ukurasa wake wa Instagram kutuma video fupi ikimuonyesha akiwashauri watu juu ya corona.

Imarkkeyz aliichukua video ile na kuikatakata kisha kuiunganisha na kuitengenezea muziki ambao umependwa sana kwani ni wa kuchezeka.

Cardi B kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika ujumbe na kusema “kulingana na ukweli kwamba wimbo wa corona virus unafanya vizuri kwenye chati za iTunes, acha nimtafute DJ ili nipate pesa zangu.”

Hata hivyo bado hakujawa na majibu yoyote kutoka kwa Imarkkeyz.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey