Sambaza

John Legend Afanya Tamasha “Insta Live”, Atangaza Album

MSANII nguli wa nyimbo za mahaba John Legend ametumia kipaji chake kuwafariji wote waliosimamisha shughuli zao na kubaki majumbani kwa sababu ya ugonjwa wa corona kwa kutumbuiza “live” kutoka Instagram.

Mwanamuziki huyo ambaye alikuwa na mkewe Chrissy Taigen walifanya tamasha hilo huku wakiwa mubashara Instagram na kwa pamoja waliimba nyimbo mbalimbali za John Legend na kisha John Legend aliamua kufunguka kuwa album yake ipo katika hatua za mwisho hivyo siku yoyote ataitoa.

Pia alisema “kila mtu yupo nyumbani, unahitaji vitu, unahitaji muziki, unahitaji runinga, unahitaji filamu, unahitaji vitu vya kukuburudisha, basi nitatoa muziki mzuri.”

Hata hivyo kulingana na hali ya kiafya kuwa sio salama sana amesema kuwa hana uhakika kama atafanya video za nyimbo hizo ila ana uhakika kuwa atafanya video za kikatuni (animation).

#Tusanue unadhani ni wakati wa wasanii wa bongo kutumia Instagram zao kuburudisha na kufariji katika kipindi hiki cha Corona?

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey