Rihanna, Jay Z Watoa Tsh Bil. 4 kwa Wahanga wa Corona
WAKATI dunia ikihaha kutafuta njia madhubuti ya kujikinga na janga la homa kali ya mapafu covid 19 inayosababishwa na virusi vya Corona, mastaa wawili wa Marekani Jay-Z na Rihanna wameingia kwenye headlines baada ya kila mmoja wao kuchangia kiasi cha Tsh Bilioni 2 kupitia taasisi zao; Shawn Carter Foundation na Clara Lionel.
Fedha hizo hizo ambazo ni jumla ya Tsh Bilioni 4, zimetolewa kwa lengo la kuwasaidia na kuwagusa madaktari, jamii na watu wasio na makazi kupata chakula vya kupambana na ugonjwa wa Corona.
Hii inapaswa kuigwa hata hapa nchini kwa mastaa na watu wote wenye uwezo kujitoa kidogo walicho nacho kuwasaidia wasicho nacho kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
Toa Maoni Yako Hapa