Simanzi: Safari ya mMwisho ya Marin Hassan wa TBC – Video
INASIKITISHA! Simanzi, vilio na majonzi vimetawala kwenye tasnia ya habari kufuatia kifo cha mwandishi mwandamizi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Marin Hassan Marin kilichotokea leo Jumatano, Aprili 1, 2020 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Marin Hassan ambaye alianza kazi TBC miaka 15 iliyopita alifariki akipatiwa matibabu hospitalini hapo baada ya kuzidiwa akiwa nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Waombolezaji wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Rioba wamejitokeza katika Ofisi za TBC Mikocheni jijini Dar na baadaye kuswaliwa katika msikiti wa Upanga kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa ajili ya maziko.
Marin Hassan atakumbukwa kwa uzalendo wake hasa kupitia kipindi alichokianzisha TBC na kukipa jina la TWENZETU DODOMA ikiwa ni kampeni ya kuhimiza kuhamia Dodoma kwa Makao Makuu ya nchi.