Sambaza

Video: Majaliwa Aelezea Mipango ya Serikali, Covid-19


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa, leo Aprili 01, 2020, ameelezea mipango ya serikali katika kipindi hiki ambacho dunia inapambana na janga la homa inayoletwa na virusi vya Corona.

Baadhi dondoo alizosema Majaliwa Bungeni:

Nampongeza Rais Magufuli kwani tumeshuhudia maendeleo makubwa nchini ikiwemo miundombinu, huduma za kiuchumi na kijamii, utawala bora, mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi pamoja na kuhamasisha uwekezaji.

Tangu kugundulika kwa ugonjwa wa Corona nchini, Serikali inafanya juhudi kukabiliana na ugonjwa huo kwa kuimarisha ukaguzi, upimaji na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini na kutoa matibabu kwa wanaothibitishwa.

Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ufufuaji wa shirika la ndege nchini (ATCL), ufufuaji wa shirika la mali za ushirika, ujenzi bwawa la ufuaji umeme, uboreshaji miundombinu ya maji, elimu na afya ni kati ya hatua za msingi katika kuhakikisha Tanzania inafika uchumi wa kati.

Vijiji vilivyounganishwa umeme nchini vimeongezeka kutoka vijiji 2118 mwaka 2015 hadi vijiji 9001 kufikia mwezi Machi, 2020 chini ya Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA).

Hadi Machi, shilingi 2020 Trilioni 1.28 zimetumika katika ujenzi wa mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere na umekamilika kwa asilimia 10.74 .

Kufikia Machi, 2020, Serikali imenunua ndege nane mpya zenye thamani ya Sh. Trilioni 1.27 na tayari malipo ya awali ya Sh. Bil 85.7 yametengwa kwa ajili ya ununuzi wa ndege zingine tatu mpya.

Bajeti ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi imeongezeka kutoka sh. Bil. 31 mwaka 2015 hadi Bil. 269 kwa mwaka 2019.

Serikali imegharamia ujenzi wa zahanati 1198, ukarabati na ujenzi wa vituo vya afya vipya 487, hospitali za Halmashauri za Wilaya 69, na Hospitali za Mikoa 10.

Serikali imeongeza mikopo katika Elimu ya Juu kutoka Sh. Bil 365 mwaka 2015 hadi Sh. Bil 450 mwaka 2019 ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu.

Changamoto ya maji imetatuliwa kwa kutekeleza ujenzi na ukarabati wa miradi ya maji 1423, kati ya hiyo 772 imekamilika ambapo miradi 710 vijijini na miradi 82 mijini.

Maduhuli ya Serikali yatokanayo na Sekta ya Madini yameongezeka kutoka Sh. Bil 205.2 mwaka 2015/2016 hadi Bil 346.6 mwaka 2018/2019, na mwaka 2019/2020 Serikali inatarajia kukusanya maduhuli ya Sh. Bil. 471.

Ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa Bil. 850 kwa mwezi mwaka 2015 hadi kufikia wastani wa Trilioni 1.3 mwaka 2019 hii ni kutokana na Serikali kuimarisha matumizi ya mifumo ya mapato kwa njia ya kielektroniki.

Tangu mwaka 2015 hadi sasa, Serikali imeokoa Sh. Bil 19.83 ya mishahara kwa kuwaondoa watumishi hewa 19,708 na vyeti vya kughushi 15,411.

 

 

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey