Davido: Hakuna Tamasha Hadi 2021, Tutawajua Watunzaji Pesa
Msanii Davido anaamini kuwa ndani ya miezi 2 au 3 ijayo kuna wasanii ambao watakuwa na hali mbaya kiuchumi.
Kauli hiyo imekuja sababu ya janga lililoikumba dunia la virusi vya Corona ambalo limepelekea shuguli mbalimbali kusitishwa ikiwemo matamasha ambayo kwa kiasi kikubwa ndiyo yamekuwa yakiingiza pesa kwa wanamuziki.
Davido alitumia ukurasa wake wa Twitter kusema hayo ambapo aliandika “Ndani ya miezi 2 au 3 tutajuwa waliokuwa wakitunza pesa, hakuna show mpaka 2021.”
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameunganisha kauli hiyo na namna wasanii wengi wa Nigeria wanavyojitolea kugawa pesa kwa wasiojiweza na wengine kukasirishwa kwanini Davido hafanyi hivyo.
Toa Maoni Yako Hapa