Sambaza

Eminem: Naona Fahari Kubwa Kuwa Baba

Msanii nguli wa kufoka Eminem ameweka bayana jinsi anavyojisikia kuwa baba wa binti yake aitwaye Hailee.

.Akiwa kwenye mahojiano na bondia wa zamani Mike Tyson, rapa huyo alisema kuwa, anafuraha sana kuwa baba sababu binti yake anamfanya ajisikie fahari na amehitimu chuo kikuu hivi punde.

Hailee ambaye amehitimu shahada yake ya Saikolojia kutoka kwenye chuo cha Michigan State University aliwahi kuzungumzia pia uhusiano wake na baba yake na kusema anakaa nyumbani kwake ambapo ni karibu na kwa baba yake (Eminem).

“Pia ninalea wapwa zangu wawili, mmoja ana miaka 26 sasa na mwingine 17, mbali na mafanikio yangu yote, huwa nikiitazama familia hii na kuona namna nimefanikiwa kuwalea, hiyo ndiyo furaha yangu” aliongeza mkali huyo wa Godzilla.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey