Sambaza

Penzi la Vanessa Mdee ‘Shata Shata’

Ni dhahiri nyota wa Bongo Fleva Vanessa Mdee ameshikwa akashikika na penzi la Mnigeria Rotimi licha ya kuwepo kwa fununu za chini chini kuwa wameachana.

Mwanadada huyo ameonyesha ni jinsi gani yupo kwenye mahaba mazito na wala hajali wala hasikii yanayosemwa na mashabiki kuwa ameutenga muziki tangu akutane na Rotimi kwenye video fupi aliyoiweka mtandaoni.

Kwenye video hiyo, Vanessa amesema kuwa “Nimekuwa kwenye tasnia kwa miaka 13 bila mapumziko, sasa nimepata muda wa kufanya ninachopenda kufanya, nimepata mapenzi mazuri, nina furaha, nina furahia maisha…”

Hata hivyo Rotimi aliingilia video hiyo na kugongelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la wanaotaka penzi hilo livunjike kwa kusema neno moja tu ambalo alilirudia mara mbili “Hatuachani, hatuachani.”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey