Jumanne Iddy: Nina Mashaka Kuna Mchezo Mchafu BSS
ALIYKUWA mshindi wa kwanza wa shindano la kuibua vipaji la Bongo Star Search (BSS), Jumanne Iddy, amefunguka mambo kadhaa kuhusu muziki wake lakini pia hakusita kutia neno kuhusu shindano hilo.
Akipiga soga na kamera za Global Tv Online, amesema alipewa zawadi ya gari aina ya Corolla 110 ambayo ndiyo zawadi anayoweza kuiongelea ila hizo nyingine amekuwa na kigugumizi kuzizungumzia.
Aliongeza kwa kusema, “Hao wengine waliofuata ndiyo walipewa pesa ila sikuwahi kufuatilia lakini hizi siku za karibuni vijana wananifuata na kuniuliza kama nilipewa zawadi kweli, sasa inanipa mashaka kwamba kuna mchezo mchafu.”
Hata hivyo, anakiri kuwa kipindi chake hakukuwa na mchezo mchafu na hata kama ulikuwepo basi ni kwa siri.
Toa Maoni Yako Hapa