Lady Jay Dee na ‘Karantini Gig’ Msimu wa Kwanza
KOMANDO wa Bongo, Fleva Lady Jay De,e ameanzisha burudani inayokufuata mpaka chumbani ikiwa ni moja ya mapambano dhidi ya Corona.
Harakati hii inayoitwa “Lady Jay Dee Quarantine Gig” ina lengo la kuhakikisha watu wanaepuka kwenda sehemu zenye msongamano mkubwa badala yake kukaa ndani na kutazama ufundi wa kuimba wa msanii huyo ili kuepusha kuenea kwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.
Katika msimu wa kwanza, Komando Jide ameimba nyimbo tatu ambazo zote amezitolea historia fupi ya namna alivyopata wazo la kuandika wimbo husika. Majina ya nyimbo hizo ni “Una tatizo gani?” “I miss you” na “Never say never.”
Toa Maoni Yako Hapa