Jeezy ni Msanii Huru Baada ya Kutoka Def Jam
Jeezy alitoa album yake ya tisa mwaka 2019 na kutangaza kuwa itakuwa album yake ya mwisho kufanya akiwa chini ya uongozi wa Def Jam na shabiki zake walidhani kuwa msanii huyo huenda anahamia kwenye uongozi mwingine mkubwa.
Mapema wiki iliyopita, Jeezy alitoa album mpya ambayo haikuwa na muhuri wa Def Jam wala uongozi mwingine wowote na kwenye mahojiano aliyofanya hivikaribuni msanii huyo aliweka wazi kuwa kwa sasa ni msanii huru na anafurahia maisha hayo.
Katika kuelezea hayo Jeezy alisema “Kwa sasa niko huru na ninafurahia kuwapa shabiki zangu kile wanachotaka bila kuwaza mlolongo mkubwa ambao ningepaswa kuupitia ili kutoa kazi yangu, kwa sasa ninatoa bila siasa na kazi zinawafikia mashabiki zangu.”
Toa Maoni Yako Hapa