Fetty Wap Ashtakiwa Kwa Kumfanyia Fujo Mwanamke
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kwa jina la Lannie amefungua mashtaka dhidi ya msanii Fetty Wap siku ya Aprili 6, 2020, ambapo alidai kuwa msanii huyo alimtishia na kumpiga ngumi na kumkaba kooni.
Hati ya mashtaka inasema kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwanamke huyo kumwambia rafiki yake jambo kuhusu sherehe ya Fetty Wap ambapo msanii huyo alisikia na kumfuata mwanamke huyo na kuanza kumfanyia fujo.
Mwanamke huyo anadai kuwa Fetty Wap alimtishia kwa maneno na kumwambia “nitakuua” na mwanamke huyo anasema aliogopa na aliamini kuwa msanii huyo angemfanyia kitendo kibaya kwa namna alivyokuwa na hasira.
Katika mashtaka hayo mwanamke huyo anaaka pesa kama fidia kutoka kwa msanii huyo, kiasi ambacho hakijawekwa wazi.
Toa Maoni Yako Hapa