Sambaza

Mshindi wa BSS Hajalipwa, Waziri Asema

KIJANA Meshack Fukuta ambaye ndiye aliyekuwa mshindi namba moja wa shindano la Bongo Star Search 2019/2020 amepeleka malalamiko yake kwenyeWizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Naibu waziri Juliana Shonza amekiri kupokea barua ya malalamiko kutoka kwa wazazi wa kijana huyo na kusema kuwa amesikitika sana kuona hakuna zawadi yoyote iliyotolewa kwa mshindi mpaka leo licha ya kuwa shindano KUmalizika tarehe 24 Desemba 2019.

amesema  amefanya mawasiliano na mkurugenzi wa shindano hilo, Madam Rita, na amekiri kuwa ni kweli hawajampa pesa yoyote mshindi zaidi ya  Sh. milioni 2 ambapo alitakiwa apewe milioni 20 na milioni 30 zitumike kumsaidia kimuziki ili kukamilisha milioni 50.

Hata hivyo mshindi wa BSS anadai kuwa amepokea milioni 1 tu na hiyo milioni 1 nyingine walipewa washiriki wote hivyo haikuwa ndani ya hesabu ya milioni 20.

Tazama Video.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey