Sambaza

Remy Ma Akataa Kumuanika Anayemuombea Mabaya

Rapa wa kike Remy Ma amewaambia mashabiki zake kuwa kuna msanii wa kike alikuwa akimuombea mabaya na alionyeshwa hadi meseji zake, hata hivyo amekataa kusema msanii huyo ni nani.

Akiwa anaongea na rafiki yake wa muda mrefu Fat Joe kwenye video fupi, Remy Ma alisema “Siwezi kusema ni nani wala kusema alisema nini sababu nikisema mtafahamu ni nani ila nilishangazwa kugundua hilo sababu tulishawahi kuzungumza na nikamwambia kuwa yeye ni mkali na mimi ni mkali na watu watajaribu kutushindanisha.”

Mwanadada huyo anasema alidhani ni watu wa tasnia ndiyo wanataka kuwagombanisha ili kuwe na ugomvi wa kimuziki lakini alipoonyeshwa meseji zake ndipo alipoamini.

Hata hivyo Remy Ma amekuwa na ugomvi wa muda mrefu na Nick Minaj na Foxy ila wadau wa muziki wanasema kuwa itakuwa sio miongoni mwa hao wawili sababu inaonekana kuwa Remy Ma hakutarajia maneno hasi kutoka kwa huyo anayemuongelea.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey