Instagram Yatoa Sababu za Kufungia Ukurasa wa Tory Lanez
MSANII Tory Lanez ameanzisha kipindi ambacho huwa kinaruka hewani kupitia ukurasa wake wa instagram kinaitwa “Quarantine Radio” ambapo huwashirikisha shabiki zake kwenye “Instagram live” yake.
Kipindi hicho kimejizolea umaarufu huku baadhi ya nyota wameshiriki ikiwemo Drake, Justin Bieber, na Chriss Brown. Pia msanii huyo huwaalika wafuasi wake kuonyesha uwezo wao wa kucheza na wengine huenda mbali zaidi kwa kuonyesha sana sehemu zao za mwili.
Hivyo wiki hii ukurasa huo ulifungiwa na instagram kufanya lolote na walitoa sababu hizi “Tunazuia maudhui Fulani ili kuilinda jamii.” Hivyo ukurasa huo utaruhusiwa kufanya kazi tena kuanzia tarehe 14 Aprili.
Toa Maoni Yako Hapa