Sambaza

Baba Yake Rihanna: Nilidhani Nitakufa, Rihanna Amenisaidia Sana

Ronald Fenty ambaye ni baba yake mzazi Rihanna amefunguka kuwa alidhani mwisho wa maisha yake umefika baada ya kuugua Corona.

Mzee huyo mwenye miaka 62 amesema kuwa mwanaye Rihanna amefanya juhudi kubwa kuhakikisha kuwa anarudi kwenye afya yake na amesimulia namna alivyompelekea mashine maalumu ya kupumulia hadi nyumbani kwake.

“Mwanangu Robyn (ambaye ndiye Rihanna) alikuwa akinijulia hali kila siku” alisema Mzee huyo, “nilidhani nitakufa nakupenda sana Robyn.”

Ikumbukwe tu Rihanna na baba yake wanatarajiwa kuingia mahakamani Juni mwaka huu ili kusikiliza hukumu ya kesi aliyoifungua Rihanna dhidi ya baba yake kuhusu matumizi ya jina Fenty.

Hata hivyo mzee Ronald amepona kwa mujibu wa madakatari baada ya kukaa karantini kwa siku 14.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey