Sambaza

P Diddy Awachezesha Rhumba Mastaa Kuchangia Corona

NGULI wa muziki wa kufoka P Diddy ametumia Instagram Live yake kuwakutanisha nyotakadhaa na kuwachezesha mziki kama njia ya kuchangia fedha ili kuwasaidia wafanyakazi wa afya katika kupambana na ugonjwa wa Covid-19.

P Diddy alianzisha shindano la kucheza muziki upitia ukurasa wake wa instagram ambapo ilikuwa ni njia ya kuwaburudisha watu na kuwaomba wachangie pesa ili kuwasaidia wafanyakazi wa afya. Miongoni mwa nyota walioingia kwenye shindano hilo ni pamoja na Justin Bieber, Naomi Campbell, Drake, Jenifer Lopez, Burna Boy, DJ Khaled, LeBron James na wengine wengi.

Hata hivyo Diddy hakuacha kuzungumza maneno kadhaa kabla ya kufunga shindano hilo na kusema “kama unashuhudia haya na hufanyi jambo muda unakwisha,” kasha akaendelea kwa kusema “hatuwezi kukaa tu na kuwaacha wafanyakzai wa afya bila msaada wowote.

Muda mfuoi baada ya kufunga shindano hilo, msanii huyo alitaja kiasi ambacho walifanikiwa kukusanaya ambacho ni dola za Marekani laki 3 ambazo ni sawa na milioni 649 pesa za Tanzania.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey